Nuru FM
Nuru FM
14 April 2026, 08:44

Ubovu wa barabara unapelekea wananchi wa kijiji cha mangawe kupata tabu ya usafiri katika kipindi cha mvua.
Na Hafidh Ally
Wananchi wa Kijiji cha Mangawe Kilichopo Kata ya Nyang’oro Wilaya ya Iringa wameiomba serikali kufanya ukarabati wa miundombinu ya barabara katika kijiji chao.
Wakizungumza na Nuru fm baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamesema kuwa barabara ya kwenda kijijini kwao ni mbovu jambo linalohatarisha usalama wao Hasa katika kipindi cha mvua kwani kuna baadhi yao waliwahi kupata ajali kutokana na changamoto hiyo.
Aidha wananchi hao wameiomba serikali kuwarekebishia Barabara hiyo huku wakimkumbuka Hayati William lukuvi ambaye alikuwa akiwapigania katika kuboresha miundombinu hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mangawe Ernest Matto amekiri kuwepo kwa changamoto ya Barabara ambapo pia waliahidiwa kuwa barabara hiyo itarekebishwa kwa kiwango cha Changarawe.
Barabara hiyo imekuwa ikitumiwa na wananchi wa kijiji cha Mangawe kwenda katika barabara kuu ya Iringa Dodoma kwa ajili ya kufanya shughuli za kijamii na kiuchumi.