Nuru FM

TRA Iringa kutatua changamoto za Kikodi

23 June 2026, 15:29

Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Maigloria Saria akizungumza na wadau wa Kodi Iringa. Picha na Hafidh Ally

TRA itaendelea kutoa elimu Kwa Jamii ili waweze kujua umuhimu wa ulipaji Kodi kitu.

Na Hafidh Ally

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Iringa imeahidi kutatua changamoto wanazokutana nazo Wafanyabiashara katika utekelezaji wa majukumu ya kikodi ikiwemo kuimarisha mazingira ya ulipaji kodi kwa hiari.

‎Hayo yamezungumzwa Leo June 23 na Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa, Maigloria Saria Katika Jukwaa maalumu la wadau lililowakutanisha wafanyabiashara, Madereva Bajaji, Madereva Bodaboda, washauri wa kodi, Wanasheria, viongozi wa dini, machifu na makundi mbalimbali ya kijamii kwa lengo la kujadili masuala ya kodi, kupokea maoni ya wananchi na kuibua mapendekezo yatakayosaidia kuboresha huduma za mamlaka hiyo.

‎B. Saria amesema Kuwa TRA itaendelea kutoa elimu Kwa Jamii ili waweze kujua umuhimu wa ulipaji Kodi kitu ambacho Mamlaka hiyo imekiona kikizungumzwa na wachangiaji wa mada.

Sauti ya Maigloria Meneja TRA

‎‎Hata hivyo Jumuiya ya Washauri wa Kodi imesema Kuwa walipakodi wamekuwa uti wa mgongo wa maendeleo ya taifa kwa miongo mitatu huku wakitaka Changamoto zilizopo katika Jamii zitatuliwe.

Sauti ya Mwenyekiti wa Washauri wa Kodi

‎Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Bajaji Mkoa wa Iringa UMABAI Bw. Melabu Kihwele amesema Kuwa TRA inapaswa kuweka Mazingira rafiki Kwa Madereva hao hasa upatikanaji wa leseni, na wanapotaka kubadili umiliki wa vyombo vyao.

Sauti ya Melabu

‎‎

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria Tanganyika TLS Kanda ya Iringa Moses Ambindwile ameipongeza TRA Kwa kuwekeza katika Mifumo ya Tehama jambo lonalosaidia wananchi kulipa Kodi kidigital.

Sauti ya Ambindilwe

‎Maadhimisho ya Miaka 30 tangu Kuanzishwa Kwa Mamlaka hiyo yameenda sambamba na kufanya Shughuli katika Wiki ya Mlipakodi inayofanyika kuanzia Juni 22 na 27, 2026.