Nuru FM
Nuru FM
10 October 2024, 15:25

Na Hafidh Ally
Kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amevitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kunakuwa na amani na usalama muda wote na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaoleta vurugu.
Serukamba amesema kuwa hawatamfumbia macho mtu yoyote yule atakaye hitaji kuvunja amani katika mkoa wa Iringa hivyo ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani na usalama vinapatikana katika kipindi hiki huku wananchi wakitakiwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kuanzia kesho tarehe 11/10/2024 Mpaka tarehe 20/10/2024.
Aidha Mh. Serukamba amewataka wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za Mitaa kusimamia ipasavyo na kuhakikisha kila mtu anapata Nafasi ya kujiandikisha na kupiga Kura katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mheshimiwa Regnant Kivinge amewataka wananchi wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Vitongoji vyake kujiandikisha katika maeneo yao ya makazi ili wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajia kufanyika Novemba 27,2024 hivyo wananchi wakiaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la awali la kujiandikisha lakini pia kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
MWISHO