SOS yataka ushirikiano mapambano ya ukatili
18 June 2026, 12:15

Shirika la Sos Children Villages limeendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia katika Jamii.
Na Joyce Buganda
Wazazi na Walezi mkoani Iringa wamekumbushwa kushirikiana katika kutokomeza matukio ya vitendo vya ukatili kwa watoto vilivyokithiri katika jamii.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika Viwanja vya Garden Afisa Miradi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la SOS CHILDREN’S VILLAGES Bi. Jesca Kawonga amesema Serikali, wadau Wazazi na Walezi wakishirikiana kwa pamoja katika kumlinda mtoto watatokomeza na kumaliza kabisa vitendo vya kikatili katika jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Iringa Afande Elizabeth Swai amewakumbusha walezi kuwalinda watoto kutokuzurula ovyo mitaani hasa katika kipindi hiki ambacho watoto wapo likizo, kwa wale watoto wa mitaani wahakikishe wanafika katika vituo Ili Kupunguza kadhia ya kuzagaa ovyo mitaani.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Benjamin Sitta, amesema vitendo vya Ukatili katika Mkoa wa Iringa vinaongezeka kwa mwaka 2025 wanawake 143 walifanyiwa ukatili watoto 138 na wanaume 6 hivyo ni vema malezi yakaelekezwa zaidi kwa watoto Ili Kupunguza vitendo hivyo.
