Nuru FM

Dkt. Mwinyi amkushukuru Rais Samia msiba wa Mwinyi

3 March 2024, 8:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega tangu Rais wa awamu ya pili, hayati Ali Hassan Mwinyi alipoanza kuugua mwezi Novemba na kupelekwa Uingereza kwa matibabu.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo Machi 3, 2024 katika hitma na dua maalum ya kumuombea kiongozi huyo ilyoandaliwa na Rais Samia katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

Aidha, Rais Mwinyi amewashukuru pia Madaktari wa Hospitali ya Mzena kwa kazi kubwa waliyoifanya kujaribu kuokoa maisha ya Mzee Mwinyi pamoja na masheikh, waalimu, ndugu, marafiki na wananchi kwa dua nyingi walizomuombea Mwinyi kwa kupindi chote alichokuwa akiugua na baada ya kufariki.