Nuru FM

Mbunge Matondo aibana serikali kuanza ujenzi wa Barabara kutoka Airport- Nyanguge

20 April 2023, 2:36 pm

Mbunge Furaha Matondo akiuliza Swali Bungeni Jijini Dodoma.

Serikali imeombwa kukarabati Barabara ya Airport kwenda Nyanguge ambayo imekuwa mbovu na changamoto kwa watumishi.

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mwanza, Mh Furaha Matondo amehoji mkakati wa serikali kuanza ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara yenye urefu wa kilomita 47 kutoka Airport kwenda Nyanguge.

Matondo amezungumza hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa wizara ya ujenzi na uchukuzi ambapo amesema barabara hiyo ni muhimu kwa sababu ni bypass ya kupita Serengeti.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemuomba mbunge huyo kuwa mvumilivu ili kuona kilichopangwa katika bajeti ya 2023/24 kwa barabara hiyo.

Waziri Kasekenya ameeleza kuwa barabara hiyo ni miongoni mwa barabara za bypass mkoani Mwanza ambapo inatoka Airport, Igombe, Kayenze hadi Nyanguge.