Nuru FM

Zaidi ya miche 2,000 yapandwa kijiji cha Ulole

3 April 2024, 9:57 am

Miti ikipandwa katika maeneo mbalimbali Wilaya ya Mufindi.

Licha ya serikali kuwa na utaratibu wa kupanda miti mara kwa mara bado kumekuwa na tabia ya wananchi kuharibu huku serikali ikapanga kuwachukulia hatua wanaokata miti ovyo.

Na Adelphina Kutika

Zaidi ya miche 2,000 ya miti rafiki na maji  imepandwa katika vyanzo vya maji kwenye vijiji vinne vinavyozunguka shamba la miti Saohill  wilayani mufindi  Mkoani Iringa ili kurejesha uoto wa asili na kuhuisha mtiririko wa maji.

Wakizungumza katika zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha maji Nyamangile kilichopo kijiji cha Ulole   ambacho kinahudumia wananchi zaidi ya elfu moja  baadhi ya wananchi wanasema uhifadhi wa vyanzo vya maji umeanza kuonesha dalili njema.

Sauti ya Wananchi wa Ulole

Kwa upande wake Mhifadhi mkuu shamba la miti SAOHILL PCO TEBBY YORAMU amesema lengo lakutoa miche hiyo nikusaidia wananchi kuendelea kuhifadhi vyanzo vya maji.

Sauti ya Mhifadhi wa Saohill

Awali akizungumza na wananchi wa kijiji cha ulole mkuu wa wilaya ya mufindi Dr. Linda Salekwa amesema serikali inaendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaobanika kuharibu vyanzo hivyo ikiwemo kufanya shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo. 

Sauti ya Dkt. Linda

Shamba la  miti SAOHILL ni miongoni mwa mashamba ishirini na nne  ya serikali ,likiwa ndio  shamba kubwa likijumuisha hekta elfu arobaini na nane na mia mbili  ni misitu ya asili na hekta elfu themanini na sita ni za miti ya kupandwa.