Nuru FM

Uingereza kuipa Ukraine makombora ya kutungulia ndege kukabiliana na Russia

28 March 2022, 9:00 am

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza ametangaza kuwa London imeamua kuipa Ukraine makombora ya kutungulia ndege ili kukabiliana na mashambulizi ya anga ya Russia.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Ben Wallace akisema hayo jana Jumapili na kuongeza kuwa, London imeamua kuipa Ukraine makombora hayo ambayo karibuni hivi yataanza kutumiwa na jeshi la nchi hiyo katika vita dhidi ya Russia.

Vita vilianza mwezi mmoja uliopita huko Ukraine baada ya nchi za Magharibi kudharau wasiwasi mkubwa wa Russia na kuendelea na siasa zao za kujiimarisha kijeshi kwenye mipaka ya nchi hiyo.

arehe 24 Februari, Russia iliingia kijeshi nchini Ukraine ikisema kuwa imelazimishwa kufanya hivyo na siasa za kibeberu za madola ya Magharibi yanayoongozwa na Marekani, na lengo lake ni kuipokonya silaha Ukraine na kuzuia wanajeshi wa NATO kujikusanya na silaha zao kwenye mipaka hiyo muhimu ya Russia.

Nchi za Magharibi zinaonesha wazi jinsi zinavyopenda kuona vita vya Ukraine vinaendelea kwa muda mrefu na shabaha yao kama wanavyosema wachambuzi wa mambo, ni kutaka kuzidhoofisha vibaya nchi zote mbili, Russia na Ukraine bila ya kujali maafa na madhara ya kuendelea vita hivyo.

Rais Vladimir Putin wa Russia amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa Mascow haina nia ya kuikalia kwa mabavu Ukraine, bali inataka kuipokonya silaha serikali ya wapenda umagharibi ya Kyiv na kuzuia kutokea vita vikubwa zaidi vya kimataifa katika siku za usoni.