Nuru FM

MMMAM yataka malezi bora kwa watoto

29 February 2024, 9:11 pm

Wadau wa Malezi makuzi ya Watoto wakizungumza kuhusu mkakati wa makuzi Bora kwa watoto. Picha Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Wadau wa watoto wilayani Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kufuatilia kwa ukaribu malezi, afya na makuzi ya watoto wanayoelekezwa na wataalam.

Akizungumza katika ufunguzi wa Program Jjumuishi ya Taifa ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya Mtoto PJT MMMAM katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi, katibu tawala wa halmashauri hiyo Bw. Frank Sichwale amesema ni vyema wadau hao wakafanya ufuatiliaji kwa kwenda kwenye maeneo husika na kuacha kukaa maofisini.

Reuben Magayane ni afisa kutoka shirika la IDYDC na watekelezaji wa mradi wa Mtoto Kwanza amesema ni vyema wadau wa watoto wakawa na ushirikiano na watendaji wa kata ili elimu hiyo ifike katika ngazi zote.

Kwa upande baadhi ya wadau wa watoto waliohudhulia ufunguzi huo wamesema mradi huo umekuja wakati muafaka kwani wananchi wanahitaji elimu sana katika malezi na makuzi ya watoto.

PJT MMMAM ni progranu jumuishi ya taifa ya malezi makuzi na maendeleo ya wazali ya mtoto imalemga kuchochea ukuaji timilifu wa mtoto kuanzia umri 0 Mpaka miaka 8 katika afua 5 ambazo ni afya, lishe,malezi yenye muitikio, ujifunzaji wa awalina ukinzi wa mtoto,