Nuru FM

Mabomu ya machozi yalindima

23 April 2021, 1:08 pm

Jeshi la polisi mkoani Iringa limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya madereva wa bajaji walikuwa wakishinikiza kuachiwa huru baadhi ya madereva waliokamatwa wakati wa mkutano baina yao na mkuu wa wilaya Richard Kasesela

Wakati wa mkutano huo uliolenga kupata ufafanuzi wa baadhi ya mapendekezo ya kurekebishwa kwa taratibu za ufanyaji kazi wa vyombo hivyo vya usafiri, Madereva hao wa bajaji wamepinga kitendo cha miongoni mwao kushikiliwa na Jeshi la Polisi wakati Mkutano ukiendelea.

Aidha kutokana na Mvutano huo baina ya Jeshi la Polisi na Madereva wa Bajaji hali ya Taharuki ikazuka baada ya kusikika mabomu ya machozi na kusababisha mkutano huo kutawanyiaka akiwemo mkuu wa wilaya ili kujinusuru na vurumai hiyo.