Nuru FM

Msigwa aahidi ushirikiano CCM

9 July 2024, 3:51 pm

Mwanachama wa CCM Peter Msigwa akiwa katika Ofisi za CCM Mkoa wa Iringa. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Zamani wa CHADEMA Kanda ya Nyasa ,Ambaye sasa ni Mwanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM)Mchungaji Peter Simon Msigwa ameahidi kuonesha ushirikiano katika chama hicho.

Mchungaji Msigwa Ameyasema hayo wakati akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za CCM Iringa Mjini na kueleza kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika kujenga chama ngazi zote na serikali kwa ujumla.

Sauti ya Msigwa

Katibu wa CCM Iringa mjini Hassan Makoba akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Iringa Mjini Said Rubeya, amesema CCM Iringa mjini imempokea Msigwa kuwa Mwanachama wao Mpya na wanaahidi kumpa ushirikiano mkubwa katika kutekeleza ilani ya chama hicho.

Sauti ya Katibu

Kwa upande wake meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kama chama watahakikisha wanamuunga mkono kwa kila jambo ili kuhakikisha wanashinda kwa kishindo kuelekea chaguzi za 2024/2025.

Sauti ya Meya

Hata hivyo Msigwa aliamua kuachana na CHADEMA na kujiunga na CCM kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kilichokutana Jijini Dar es salaam Juni 30, 2024 kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.