Nuru FM

Mkoa Wa Iringa Kuweka Mkakati Maalum Kuunusuru Mto Ruaha

12 November 2022, 8:04 am

KAMISHNA Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki  amesema  mto Ruaha mkuu (Great Ruaha)hautirishi maji kama ambavyo ilivyokuwa miaka ya nyuma na kusababisha madhara makubwa ya wanyama pori waliopo katika hifadhi hiyo.

 

Akizungumza na waandishi Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki alisema kuwa takribani kilometa 164 za mto huu ambao unapita ndani ya hifadhi ya mto huu wa Ruaha,baada ya kupita ndani ya hifadhi basi mto huu hutiririsha maji yake katika bwawa la Mtera , Kidato na Bwawa la Mwalimu Nyerere na ni mto muhimu sana kwa hifadhi ya Taifa Ruaha.

 

Ole meing’ataki alisema kuwa mto huo kushindwa kutiririsha maji linasababisha maji machache yaliyopo kwenye madimbwi na mabwawa ya asili kwenye mto kupata joto ambalo Sasa huleta madhara kwa viumbe hai ambavyo vinaishi kwenye maji hayo.

Ole Meing’ataki alisema kuwa Wanyama wakinywa maji kwenye madimbwi hayo basi vile vimelea vya magonjwa husambaa kwa urahisi, jambo lingine ambalo walikuwa wakiliona huko nyuma ni majangiri ambao walikuwa wanaingia katika baadhi ya maeneo ya hifadhi wanaweza kufika kwenye maeneo yenye maji na madimbwi kama haya na kuweka mitego yao na kuwanasa wanyama lakini pia wakati mwingine wanaweza kutumia sumu inayoweza kuua wanyama mbalimbali

 

Alisema kuwa wanyama wanaishi kwenye maji hasa mamba, viboko na samaki wanaishi katika mto huu kwa sasa wana hali ngumu kwasababu hali ya maji ni mbaya maana hadi sasa mto huo hautiririshi maji yake , mto umeacha kutiririsha maji yake na maeneo machache yaliyobaki ni maeneo yenye madimbwi ambako kuna maji ambayo yanatumiwa na wanyama wote wanaofika katika maeneo haya

 

“Ni maeneo ambayo machache sana yamebaki katika mto huu na ukitizama kwa karibu maeneo haya maji yaliyoko
kwenye haya madimbwi hata rangi yake imebadilika sio maji ya kawaida kwa maana ni maji machafu kwasababu wanyama wengi wanatumia na wanatumia katika maeneo haya wanaishi humo humo, wengine wanafia humo humo, wanajisaidia humo humo,wengine wanakuja wanakanyaga kwa hiyo maji ni machafu kwa ujumla”alisema
Meing’ataki

 

Ole meing’ataki alisema kuwa Maji hayo sio mazuri kwa uhai wa wanyama na wanyama hawana namna kwasababu maeneo machache yaliyobaki kwa hiyo wanyama wanakusanyika katika maeneo haya kwa ajili ya kupata maji na Uhai wa hifadhi hii kama nilivyosema unategemea uwepo wa mto Ruaha na hasa maji yanayotiririka kutoka kwenye bonde kubwa la Usangu ambalo liko ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha.

 

Ameongeza kuwa mazingira ya hifadhi yanaharibika kwa maana ya wanyama wanapokusanyika eneo dogo wanatumia kile kilichopo kwa kufuata maji kwenye madimbwi hayo, hivyo kuleta uharibifu mkubwa
wa mazingira ndani ya hifadhi tofauti na kama maji yangekuwa mengi wanyama wangekunywa na kuendelea na shughuli zao.

 

“Kwa hiyo ukitizama au ukitembelea kando kando ya mto Ruaha mkuu (Great Ruaha) kwa sasa uoto wa asili sasa umeanza kuharibika kutokana na wanyama kuja kwa idadi kubwa katika eneo hili ambapo madhara yake kwa baadhi ya wanyama na hasa jamii ya samaki wamekuwa wanakufa kutokana na maji yaliyopo yanakuwa ni machafu na hali ya hewa pia hapa ni ya joto kipindi hiki” alisema Meing’ataki

 

Alisema kuwa walipofanya uchunguzi kwenye madimbwi haya walibaini samaki wanakufa kwasababu ya kukosa hewa ya Oxgen ambayo inafanya waishi kwenye maji lakini pia wameona katika kipindi hiki wanyama wanatafuta maeneo mengine ya kupata maji ya kutumia na wanatoka nje ya hifadhi na wanasababisha migogoro kati ya binadamu na wanyama kwa kuharibu mazao na mali nyingine za binadamu.

 

Aidha Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki alisema kuwa wanaona kuna uchepushaji mkubwa wa maji katika maeneo mbalimbali ambapo unakuta baadhi
ya wananchi wameanzisha mashamba na hawajali kwamba haya maji yanahitajika kwenye matumizi ya maliasili kama hizi za wanyama pori lakini pia kwa ajili ya uzalishaji umeme na matumizi mengine ya kiuchumi hasa kupitia eneo hilo.

 

“Kwa hiyo huu mto Ruaha mkuu (Great Ruaha) naweza kusema ni muhimu ni muhimu kwa mtazamo huo kwamba kweli ni kivutio kwasababu maliasili ambazo tunazo wanyamapori wakubwa na wadogo wanapatikana katika maeneo haya na ukiangalia utalii unaofanyika katika hifadhi kwa kiasi kikubwa kuna njia nyingi za utalii ambazo zinakwenda kando kando ya huu mto Ruaha kwasababu wageni wanaweza kuona wanyama kwa karibu”alisema
Meing’ataki

 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego amesema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa imejipanga
kuhakikisha inatafuta mkakati sahihi ya kunusuru mto Ruaha mkuu (Great Ruaha) kutokana na uharibifu wa kimazingira ambao unafanywa na binadamu katika vyanzo vya maji kwenye vyanzo vyote vya mto huo.

 

Dendego alisema kuwa kila mtu aliyefika katika hifadhi ya Taifa Ruaha namna gani mto huo ulivyokauka na
hakuna maji ambayo yanatiriri katikamto Ruaha mkuu(Great Ruaha).

 

Alisema kuwa watawaondoa na kuwakamata wananchi wote ambao wanaoharibu vyanzo vya maji na wanaotumia maji ya mto huo kinyume na sheria inavyotaka juu ya matumizi ya maji ya mto Ruaha mkuu(Great Ruaha).

 

alimalizia kwa kuwapongea viongozi wa serikali ya mkoa wa Mbeya kwa kuanza kuchukua hatua za kuwaondosha wafugaji kwenye hifadhi na kwenye vyanzo vya maji ili kuukoa Great Ruaha kuahidi sasa ni
zamu ya Iringa kuchua hatua