Nuru FM

CCM Iringa: Rais Samia ametoa uhuru wa kidemokrasia

26 March 2024, 10:02 am

Katibu wa siasa,uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa Joseph Ryata akizungumzia mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan. Picha na Mwandishi wetu.

Miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeimarisha demokrasia kwa vyama vya siasa.

Na mwandishi wetu

Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimesema Rais Dr Samia suluhu Hassan ametoa uhuru wa kufanya siasa kwa vyama vyote.

Akizungumza na mwandishi wa habari katibu wa siasa,uenezi na mafunzo mkoa wa Iringa Joseph Ryata alisema kuwa Rais Dr Samia suluhu Hassan katika kipindi cha miaka mitatu ametoa uhuru mkubwa kwa vyama vyote vya siasa kufanya siasa kwa uhuru.

Ryata amesema kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kinabanwa kufanya siasa katika kipindi hiki cha Rais Dr Samia na mara kwa mara amekuwa akikaa meza moja na wapinzani kujadili masuala ya kisasa kwa maendeleo ya Tanzania.

Alisema kuwa Rais Dr Samia amekuwa habagui vyama vya siasa kwa kufanya majadiliano kuanzia chama kidogo kwenye ushawishi hadi chama cha upinzani chenye ushawishi mkubwa kwa mstakabali wa maendeleo ya taifa la Tanzania.

Ryata alisema kuwa Rais Dr Samia ni tunu ya taifa kwa kuongeza nchi kizalendo zaidi kwa kuwajali watanzania wote bila kujali itikadi, kabila dini wala mlengo wa kisiasa.