Nuru FM

Ritta Kabati trust fund kunyanyua mchezo wa Basketball kwa walemavu

24 March 2024, 11:14 am

Mratibu wa Ritta Kabati trust fund Mwenye T-shirt ya njano akiwa katika studio za Nuru FM kuzungumzia kuhusu mazoezi kwa watu wenye ulemavu. Picha na Ayoub Emanuel

Licha ya Mchezo wa Kikapu kupendwa na Watu wa rika tofauti, mchezo huo umeonekana kupendwa zaidi na watu wenye ulemavu baada ya Taasisi ya Ritta Kabati Trust Fund kuwawezesha kufanya mazoezi na kuunda timu imara.

Na Hafidh Ally

Taasisi ya Ritta Kabati Trust Fund imeahidi kushirikiana na Shirikisho la Vyama Vya Watu wenye Ulemavu mkoa wa Iringa (SHIVYAWATA) kukuza ushiriki wa michezo kwa watu wenye ulemavu mkoa wa Iringa.

Hayo yamesemwa na mratibu wa Taasisi hiyo, Halfan Akida wakati
Timu ya mpira wa kikapu kwa kutumia viti Mwendo mkoa wa Iringa ikiendelea na mazoezi yake katika viwanja vya Garden, Posta, Manispaa ya Iringa.

Amesema taasisi hiyo imejipanga kuhakikisha Mkoa wa Iringa mchezo huo unakua na timu za michezo kwa watu wenye ulemavu pamoja na kuandaa mabonanza ya michezo kwa watu wenye Ulemavu.

Akizungumza katika mazoezi hayo mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Shomari Shabani amesema wanaipongeza taasisi ya Ritta Kabati kwa kuendelea kuhamasisha michezo kwa watu wenye ulemavu mkoa wa Iringa.

Aidha Shabani ametoa wito kwa watu wenye ulemavu kujitokeza kushiriki michezo kwa kuwa ni sehemu ya mazoezi na ajira.