Nuru FM

Madereva Bajaji wadokozi waonywa

6 May 2024, 11:36 am

Picha ya Madereva Bajaji Manispaa ya Iringa.

Tabia ya wizi imekuwa ikipigwa vita hasa baada ya abiria kusahau mizigo yao ndani ya vyombo vya moto.

Na Agness Leonard

Madereva bajaji mkoani iringa wametakiwa kuwa waaminifu pindi abiria anaposahau mzigo kwenye chombo cha usafiri.

Hayo yamezungumzwa na Makamu Mwenyekiti wa wamiliki wa Bajaji Mkoani iringa PETER HAULE na kuongeza kuwa kumekuwa na tabia ya madereva kutokuwa waaminifu pindi abria wanaposahau mizigo yao.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti

Amesema abiria ambao ni wateja wao wamekuwa wakisahau kushuka na mizigo  wanayoingia nayo kwenye chombo cha usafiri huku wakiwataka abiria kukariri namba za bajaji ili waweze kupata mizigo yao.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti

Kwa upande wao baadhi ya madereva wa bajaji Manispaa ya Iringa wamewataka abiria wao kutokuwa na tabia ya kuweka mizigo nyuma ambapo baadhi ya abiria wamekuwa wakiibiana wao kwa wao.

MWISHO