Nuru FM

Nyumba Ya Familia Ya Watu Wenye Ulemavu Lulanzi Mkoani Iringa Yafikia Hatua Ya Kuezekwa Bati

9 June 2022, 5:55 pm

Ujenzi wa nyumba ya watu watatu wa familia moja wenye ulemavu katika kijiji cha lulanzi kata ya Mtitu Wilaya ya Kilolo Mkoani iringa umefikia hatua ya kuezekwa bati.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo Wilson Nyangile amesema kuwa nyumba hiyo inayojengwa chini Taasisi ya Balozi wa Utalii Tanzania Iabella mwampamba ya Isabella African Foundation imefikia hatua nzuri na vifaa vyote vimeshanunuliwa na huenda mradi huo ukakamilika kabla ya mwezi wa saba.

Amesema kuwa kazi hiyo inayofanywa na Shirika la RDO Wilaya ya kilolo imeenda kwa haraka kutokana na mchango Milioni Tano ambao aliutoa Waziri wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa baada ya kununua mahitaji yote ikiwemo bati, Mbao, Misuramari, saruji, mchanga, na gharama za usafirishaji.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mtitu Mh. Rahman Mkakatu amepongeza hatua ambazo zimefikiwa huku akiwataka wadau wa maendeleo kuendelea kutoa michango kwa kuwasiliana na Mratibu wa zoezi hilo Isabella mwampamba kupitia namba 0762 756046 ili waweze kupewa utaratibu wa kuoa michango yao.

Naye Mkuu wa chuo cha RDO Wilaya ya Kilolo Lameck Mlamka amesema kuwa chuo chao kimeamua kujenga nyumba hiyo kwa gharama nafuu huku wakiahidi pia kufunga mfumo wa umeme na maji mara baada ya nyumba hiyo kukamilika hatua ya kuezeka bati.

Awali Mmiliki wa Taasisi ya Luganga Hardware iliyopo Wilaya ya Kilolo Bw. Genero Lucas Lukosi amesema kuwa taasisi yake imeshiriki kupeleka vifaa vya ujenzi katika familia hiyo ya watu wenye ulemavu huku akiwashukuru viongozi wa serikali wakiongozwa na Waziri Mkuu kwa kushiriki katika mradi huo.

Walemavu hao wana uhitaji wa kuvutiwa maji, kujengewa nyumba ya kisasa, kupatiwa vifaa vya malazi, vifaa vya jikoni na gharama za chakula matibabu ambapo gharama zote ni shilingi milioni 20 na FEDHA zote zinapolokelewa kupitia acaount namba ya CRDB iliyosajiliwa kwa jina la Isabella African Foundation ya 015C621885600 huku Miradi hiyo ikitarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mwezi Mei mpaka Julai 2022.