Nuru FM

Serikali kuimarisha sheria ya kodi

6 February 2023, 10:33 am

Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Paul Walalaze. Picha na Joyce Buganda

Tunaomba kuboreshwe kwa baadhi ya sheria za kodi hapa Nchini ambazo zinawabana wafanyabiashara.

Na Joyce Buganda

Serikali imeombwa kuendelea  kuzingatia upya  sheria za kodi ili kuimarisha uzalendo  na ulipaji kodi wa hiari.

Hayo yamezungumzwa na naibu katibu Mkuu wa  Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania   BW. JAKSON KALOLO  amesema  baadhi ya taaratibu na Sheria za ulipaji kodi sio rafiki  na zinakwamissha jitihada za kuipa kodi kwa wakati.

Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Jackson Kalolo

PAUL WALALAZE  ni Meneja wa TRA mkoa wa iringa  amesema  mamlaka hiyo inashirikiana  vyema na wafanyabiashara na kuwaomba kuendeleza ushirikiano huo ili kukuza uchumi wa nchi.

Walalaze amesema kuwa TRA iko tayari kutatua changamoto za Kibiashara kwa wafanyabiashara Mkoani Iringa.

“Sisi TRA Tunafanya kazi kutokana na malengo ambayo tumejiwekea na kwa kweli tunawapongeza wafanyabiashara ambao wamekuwa mstari wa mbele kulipa Kodi” alisema Walalaze

“Sisi TRA Tunafanya kazi kutokana na malengo ambayo tumejiwekea na kwa kweli tunawapongeza wafanyabiashara ambao wamekuwa mstari wa mbele kulipa Kodi” alisema Walalaze

Hivi karibuni akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa waziri wa uwekezaji  viwanda na biashara EXZAUD KIGAHE  alisema kuwa serikali imeendeleza kuboreha sera na miongozo mbalimbali  ili kurahisisha ulipaji  wa kodi na kuimarisha sekta binafsi nchini.