Nuru FM

DC MOYO ATOA MWEZI MMOJA KWA IDARA YA MIPANGO MIJI KUMALIZA MGOGORO WA KIUMAKI NA WANANCHI MKIMBIZI.

28 October 2022, 4:56 pm

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametoa mwezi mmoja idara ya mipango miji kuhakikisha wanatatua mgogoro ya mipaka katika eneo la mlima Igeleke uliopo kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa baina ya wananchi na kikundi cha uhifadhi wa mazingira KIUMAKI.

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara,mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa idara ya mipango
miji inatakiwa kufanya kazi haraka ya kuitambua mipaka ya mlima Igeleke na maeneo ya wananchi.

Moyo alisema kuwa amegundua kuwa kuna mapungufu waliyoyabaini katika nakala ya mkataba uliowapa mamlaka KIUMAKI kujihusisha na uhifadhi katika eneo hilo hivyo ni muhimu ukapitiwa ili kujiridhisha.

Alisema kuwa kufuatia mapungufu ya kimkataba ikiwemo kuwepo kwa Mashaka ya uhalali wa mkataba huo baina ya Ofisi ya  Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa na KIUMAKI na kuamuru mkataba huo kuwasilishwa katika ofisi mapema kesho asubuhi Ili uweze kupitia na kamati ya Ulinzi

Lakini pia mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliamuru kukamatwa Kwa Mtu yeyote atakayebainika kufanya shughuli za kibinaadam katika hifadhi ya Igeleke wakati huu serikali ikishughulikia Mgogoro baina ya Wananchi na kikundi Cha uhifadhi Cha KIUMAKI.

Moyoalimazia kwa kuwaomba wananchi wa mtaa wa Kihesa Kilolo A  na B kuwa na subira wakati serikali ya wilaya ikiwa inautafutia ufumbuzi mgogoro huo.

Kwa upande wa wananchi wa Kihesa Kilolo A na B walisema kuwa kikundi cha KIUMAKI kimepora ardhi ya eneo hilo kwa kutumia mabavu kwa madai kuwa kikundi hicho kinachojihusisha na utunzaji wa Mazingira katika Mlima Igeleke yalipo makumbusho ya michoro ya kale.

Fausta Timoth Kitindi ni bibi anayekadiliwa kuwa na zaidi ya miaka miaka 70 alisema kuwa Amekuwa akikumbana na bughudha ya Mgogoro huu huku eneo aliloachiwa na wazazi wake pamoja sehemu kaburi kutajwa na kikundi hicho kuwa ni eneo lililo chini ya Hifadhi.

Awali Katibu wa KIUMAKI Filipo Mkwama alisema walichukuwa maeneo hayo na kuanza kuyaifadhi kwa kufuata
taratibu na sheria za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kuingia mkataba baina ya kikundi hicho na uongo wa Manispaa ya Iringa.

Hata hivyo Kaimu Afisa Ardhi wa Manispaa ya Iringa  Priscus Shirima ameshauri baadhi ya masuala muhimu kufanyika huku akitoa hakikisho la kuanishwa Kwa mipaka ya eneo hilo.