Nuru FM

Dkt.Mpango Awasili Nchini Kenya Kumuwakilisha Rais Katika Mazishi Ya Hayati Mwai Kibaki

29 April 2022, 9:17 am

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Aprili 2022 akiwasili  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta uliopo Nairobi nchini Kenya alipoenda  kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki.

Makamu wa Rais ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM-Bara) Komredi Abdulrahman Kinana