Nuru FM

Serikali Kukamilisha Miradi Ya Umwagiliaji Mkoga Na Kitwiru Mkoani Iringa

6 April 2022, 6:29 am

Serikali kupitia Wizara ya Kilimona Umwagiliaji imetoa kipaumbele kwenye miradi ya umwagiliaji iliyopo Mkoani iringa ili wananchi waweze kulima kilimo cha biashara.

Hayo yamezungumzwa Jijini Dodoma  na Naibu waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Antony Mavunde aalipokuwa ajibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dr. Ritta Kabati aliyetaka kujua ni lini serikali itakamilisha Mradi wa Mkoga na Kitwiru kwa kutoa fedha ili kukuza uchumi wa wananchi wa eneo hilo?

Mbunge Kabati alihoji na kuongeza kuwa endapo Miradi hiyo itakamilishwa, wananchi wanaozunguka Miradi hiyo watapata ajira kupitia kilimo.

Akijibu swali la Mbunge Kabati, Mh Mabunde amesema kuwa serikali imetuma tume ya uhakiki kujua ni gharama kiasi gani zinahitajika ili kukamilisha miradi hiyo.

Amesema kuwa kuelekea agenda ya kukuza kilimo cha umwagiliaji tayari serikali imeongeza bajeti katika wizara ya kilimo kutoka bilioni 17 hadi bilioni 51.

Aidha ameongeza kuwa kipaumbele kikuu cha serikali kupitia wizara ya kilimo ni kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinakuwa agenda kuu kwa kukamilisha miradi yote ya umwagiliaji.