Nuru FM

Waonywa kuacha kuwatumikisha watoto katika uchungaji wa mifugo

24 April 2024, 10:27 am

Picha ikionesha Mtoto akiwa katika kazi ya kuchunga mifugo. Picha kwa msada mtandaoni

Licha ya serikali kuweka mazingira rafiki kwa watoto kusoma bado kuna baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwapeleka watoto kuchunga mifugo.

Na Joyce Buganda

Jamii ya wafugaji Kata ya Kiwele Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetakiwa kuwapeleka watoto wao shule badala ya kuwatumikisha katika kazi za kuchunga mifugo.

Akizungumza katika kikao cha wafugaji Diwani wa kata hiyo Felix Waya kilichoketi kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi amesema kuwa kutakuwa na operesheni ya kuwasaka watoto wenye umri wa kuanza darasa la kwanza lakini wanafanyishwa shughuli za uchungaji na walioolewa mara baada ya kuhitimu darasa la saba ili wapate haki yao ya elimu.

Sauti ya Diwani Felix

Naye Afisa Maendeleo kata ya Kiwele Magdalena Mkwawi amesema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto wao wafanye vibaya katika mitihani yao ya darasa la saba ili wafeli kisha waolewe.

Sauti ya Afisa Maendeleo

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa hali hiyo imepungua tofauti na awali na wameeleza sababu ni wazazi kuwakatisha tamaa watoto kwa sababu ya uchumi ni mgumu.

Sauti ya wananchi Kiwele

MWISHO