Nuru FM

TAKUKURU kufuatilia matumizi ya milion 10 Iringa

12 March 2024, 11:01 am

Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akizungumzia katika baraza la madiwani Iringa. Picha na Godfrey Mengele

Matumizi ya zaidi ya Milioni 60 katika ujenzi wa stendi ya mabasi ya Igumbilo yamemuibua Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa kujua uhalali wa Matumizi.

Na Godfrey Mengele

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amelazimika kuiagiza mamlaka ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kuingilia kati kushughulikia suala la milioni 60 ambayo matumizi yake hayaeleweki yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la mapokezi katika stendi ya Mabasi ya Igumbilo.

Meya Ibrahim Ngwada ameyasema hayo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Iringa lililokutana kujadili taarifa za utekelezaji na utendaji kazi katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2023/2024 na kuongeza kuwa baraza hilo limeidhinisha fedha mara kadhaa lakini matumizi yake hayaeleweki na jengo bado halijakamilika katika stendi hiyo.

Sauti ya Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa

Kufuatia hali hiyo Meya Ngwada amesema baraza lina mashaka juu matumizi ya fedha zilizokuwa zinatolewa hivyo kuvitaka vyombo vya usalama kuanza uchunguzi ili kubaini matumizi sahihi ya fedha hizo.

Katika hatua nyingine Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amewataka wataalam wa halmashauri hiyo kufuata maagizo yanayotolewa ikiwamo utekelezaji wa miradi mbalimbali.