Nuru FM

Wazazi Sababu Mimba za Utotoni Iringa

17 February 2023, 4:53 pm

Wazazi na walezi mkoa wa Iringa watajwa kuwa chanzo cha mimba za utotoni kwakutozungumza na watoto wao kwa uwazi pindi yanapotokea mabadiliko ya kimwili

Na Fabiola Bosco.

Wazazi na walezi mkoani Iringa wametakiwa kuzungumza na watoto kwa uwazi pindi yanapotokea mabadiliko ya kimwili ili kuwalinda na mimba katika umri mdogo

Akizungumza na Nuru Fm Hiyad Sweddy mzazi aliyetoa elimu kwa watoto wake amesema kuwa mzazi anapaswa kuwa muwazi kwa mtoto huku ushiriki wa mzazi wa kiume ukihitajika zaidi .

Hiyad Sweddy mzazi aliyetoa elimu kwa watoto wake akielezea umuhimu wa wazazi hasa wa kiume kuwa wazi kwa watoto

kwa upande wake Farid James amesema kuwa amekuwa akipatiwa elimu na mzazi wake huku akibainisha ukali kwa wazazi pamoja na kutokuwa na ukaribu baina ya mzazi na mtoto inaweza pelekea mimba katika umri mdogo

Farid James akieleza tabia ya ukali kwa wazazi inavyowapelekea watoto katika mimba za utotoni

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoani Iringa Elizabeth Swai amefafanua namna mzazi anapaswa kufanya ili kumlinda mtoto wa kike na mimba katika umri mdogo

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Iringa Elizabeth Swai akieleza kwa kina zaidi kuhusu mimba za utotoni