Nuru FM

Trees for the future mkombozi kwa wakulima

8 May 2024, 12:24 pm

Mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo akipata cheti kutoka Taasisi ya Trees fore the future. Picha na Joyce Buganda

Zaidi ya wakulima 1000 mkoani Iringa wamenufaika na mafunzo kutoka Taasisi ya Trees for the future.

Na Joyce Buganda

Taasisi ya TREES FOR THE FUTURE imewataka wahitimu wao kufanya kwa vitendo mafunzo waliyoyapata ili yaweze kuwa na tija na manufaa kwao.

Akizungumza wakati wa mahafari ya pili yaliofanyika katika ukumbi wa siasa na kilimo mkoani Iringa Mratibu wa TREES FOR THE  FUTURE mkoa wa Iringa Daud   Fonga amesema hiyo ni mahafari ya pili na kwa mwaka huu zaidi ya wahitimu 1000 wamenufaika na mafunzo hayo.

Sauti ya Mratibu

Grint Godfrey Mwimanzi ni balozi wa Mazingira kutoka ofisi ya makamu wa Rais Mazingira amesema serikali inashirikiana vizuri na taasisi kama TREES FOR THE FUTURE na CLINTON DEVELOPMENT ili kukabiliana na tabia nchi hasa kilimo, ufugaji na kufanya jamii iungane pamoja. 

Sauti ya Balozi

Aidha afisa mazingira mkoa wa Iringa ambae alikuwa mgeni rasmi amesema mzaidi yakoa wa Iringa una historia ya kilimo hivyo mradi huo umekuja sehemu husika  pia  kumefanya ushirikiano baina ya mashirika ya uma na binafsi kushikamana kwa pamoja katika  uboreshaji wa lishe ni mkakati wa mkoa kutokana na changamoto ya udumavu tulionayo lakini mazingira ni wajibu kwa kila mtu.

Sauti ya Afisa mazingira

Wakisoma risala wakati wa mahafali hayo wahitimu hao wamesema elimu walioipata wataiambukiza kwa wengine ili ienee zaidi kwani wameiva kwa miaka miwili hiyo wamehakuwa pia wanaiomba serikali ya mkoa kuona namna ya kuwasidia katika chngamoto ya ukosefu wa maji kwnye bustani misitu.

Sauti ya Wahitimu

TREES FOR THE FUTURE NA CLINTON DEVELOPMENT  ni mashirika yanayoshirikiana katika kuendesha mafunzo hayo kwa wakulima na wafugaji huku lengo lao kuu likiwa ni kuongeza kipato kupunguza udumavu kwa jamii kwa kulima mazao mchaganyiko, miti ya matunda na mbogamboga lakini pia kutunza mazingira kwa kupata miti ili kuzuia mmomonyoko na kupanda miti kupendezesha mazingira.