Nuru FM

Andikeni habari zinazogusa jamii

12 March 2024, 5:34 pm

Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na maafisa wa jeshi la Polisi wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Waandishi wa habari mkoani Iringa wametakiwa kuachana na uandishi wa kawaida na badala yake wajikite kuandika habari za wananchi ili kuwaongezea heshima katika jamii.

Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Iringa Press Club (IPC) Frank Leonard katika mdahalo wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari na jeshi la polisi. Amesema lengo kubwa na kufanya mdahalo huo ni kukuza mahusiano mazuri kati Jeshi la Polisi na waandishi wa habari.

“Waandishi wa habari badilikeni namna ya uandishi wenu acheni uandishi wa kawaida na badala yake mjikite kuandika habari za wananchi huku mkitumia weledi wenu katika uandishi kwani kwa kufanya hivyo kutawaongezea heshima katika jamii. “Alisema Mwenyekiti.

ALLAN BUKUMBI ni Kamishina, Msaidizi,Mwandamizi na kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa amesema vyombo vya habari vina wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata habari kuhusu wajibu na majukumu hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Vyombo vya habarivina wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi hasa kwa mwaka huu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa lakini pia upembuzi yakinifu wa habari kabla ya kuzipeleka kwa wananchi wapo baadhi wanapotosha taarifa”

Kwa upande wao baadhi waandishi wa habari waliohudhuria mdahalo huo wamesema wanashukuru kwa elimu wanaoipata kwenye midahalo hiyo kwani inazidi kuwafanya wawe imara katika taaluma yao.

Ikumbukwe kuwa mdahalo huo wa ulinzi na usalama kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi umedhaminiwa na international media support IMS kupitia umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania UTPC.