Nuru FM

Wazazi Wapeni nafasi watoto kushiriki michezo

5 April 2023, 12:41 pm

Wazazi wametakiwa kutenga muda wa kushiriki katika michezo baada ya masomo na kuwanunulia vifaa vya michezo ili wawe na afya bora.

Na Adelphina Kutika

Wazazi na  wazazi Manispaa ya Iringa wametakiwa  kuwapa nafasi watoto kushiriki katika michezo ili kuibua vipaji walivyo navyo watoto na kuviendeleza ili viweze kuwa msaada kwa maisha ya baadae ya mtoto.

Wito huo umetolewa na Mwalimu wa Michezo katika shule ya Msingi Kilongayena iliyopo kata ya Ruaha Chrispilin Nziku  ameeleza kuwa ni jukumu Lao wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kushiriki katika michezo baada ya masomo na kuwanunulia vifaa vya michezo ili watoto waweze kuibua vipaji walivyo navyo huku akiikiomba serikali kuboresha miondombinu ya michezo katika shule hiyo.

“Michezo inasaidia watoto wanakua na afya njema, na kuibua vipaji ambavyo vitawasaidia wao na taifa” alisema Nziku.

Samweli  Chapwaya  na hellen Nombo ni viongozi wa shule ya msingi Kilongayena amewashauri wazazi kuzingatia suala la michezo kwa kuwa inasaidia kuwajenga kiakili na kiafya pia.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema wazazi wasiwazuie watoto wanapoonesha vipawa vyao ili kutimiza malengo yao pindi wanapohitimu masomo.