Wahariri na waandishi wa habari wa radio jamii wakifuatilia mafunzo
Nuru FM

Wahariri wa Radio Jamii wapigwa msasa

30 January 2023, 9:28 am

Wahariri na waandishi wa vyombo vya habari vilivyopo chini ya Mtandao wa Redio Jamii Tanzania TADIO wameanza mafunzo ya namna ya kuandaa kuhariri na kuzituma habari kupitia tovuti ya mtandao huo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyoanza Jan 30 mpaka jan 31 mwaka 2023 Mwenyekiti wa TADIO John Baptist amesema kuwa ni vyema wahariri hao wakazingatia mafunzo hayo ili waweze kuandaa habari zenye maslahi kwa jamii.

Wahariri na waandishi wa Redio Jamii 9 wakiwa wakipokea mafunzo Katika Ukumbi wa Jamirex Hotel uliopo Mwenge Jijini Dar Es salaam.

Amesema kuwa lengo la kuwaita Wahariri hao kuwapa mafunzo hayo ni kwa sababu ndio watendaji ambao wana jukumu la kuhakiri habari hizo katika tovuti ya TADIO.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika ukumbi wa Jamirex Hotel uliopo Mwenge Jijini Dar es salaam ambapo jumla ya vyombo vya habari 9 vyenye wawakilishi wawili kwa kila chombo vimeshiriki.