Nuru FM

ALLY MTERA: Changamoto ya hedhi kwa wanawake chanzo cha kutopata Ujauzito

6 April 2022, 6:34 am

Imeelezwa kuwa kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi kwa wanawake hupelekea kushindwa kupata ujauzito na kupata  maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Tiba asili kilichopo Chalinze Mkoani Pwani cha Ilham Herbal Clinic Bw. Ally Said Mtera alipokuwa akizungumza na Nuru fm na kuongeza kuwa kujua mzunguko wa hedhi kwa mwanamke kutakusaidia kupata ujauzito uliopangiliwa  na kuepuka kupata ujauzito ambao haukupangiliwa.

Ally amesema kuwa Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na Msongo wa mawazo, Mabadiliko ya kisikolojia,Uvimbe kwenye kizazi, kwenye Ovary na katika mirija ya Uzazi.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na Matatizo kwenye vifuko vya mayai,Mimba kuharibika, Matatizo ya  U.T.I na Fangasi ya mda mrefu ambayo hupelekea Kutokwa na uchafu ukeni mara kwa mara na Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Mtera amesema kuwa kituo chake kimekuwa mkombozi kwa kutoa dawa za asili zenye homoni ambazo husaidia kurejesha mzunguko sahihi wa hedhi kwa wanawake.

Ameongeza kuwa mwanamke anapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri akafika katika kituo chake cha Ilham herbal Clinic na atakutana  madaktari bingwa na wataalamu wengine ambao watamsaidia kufanya uchunguzi wa kutosha kubaini changamoto na kumpatia suluhisho la kudumu.

Amesema kuwa wameweka utaratibu wa kutoa huduma kwa wananchi waliopo nje ya mkoa huo kwa kuwatumia dawa huku akiwataka kuwasiliana naye kupitia namba 0653-796582.

Kituo cha Ilham Herbal Clinic kimekuwa kikitoa huduma kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya afya kwa kutumia miti shamba.

MWISHO