Nuru FM

Rhythm Foundation yatoa msaada kwa wagonjwa hospitali ya Ipamba

15 February 2024, 7:23 pm

Wadau kutoka taasisi ya Rhythm wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa msaada Hospital ya Ipamba. Picha na Fabiola Bosco

Na Fabiola Bosco

Taasisi ya Rhythm Foundation nchini Tanzania imetoa msaada kwa wagonjwa katika hospitali ya Ipamba mkoani Iringa katika siku ya wapendanao duniani ambayo huadhimishwa kwa matukio tofauti ulimwenguni.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo Shariffa Salum Mdau kutoka Rhythm Foundation amesema kuwa Valentine si siku wapendanao tu bali ni siku ambayo inapaswa kutumika kwa kuwakumbuka watu wenye uhitaji kwa kuwaonesha upendo .

“Mimi nina furaha sana nimeweza kufika hapa Ipamba kusherehekea siku ya wapendanao na wapendwa wenzetu na kikawaida siku ya wapendanao wanasherehekea watu walio kwenye mahusiano au ndoa lakini kwenye jamii yetu kuna wagonjwa wazee akina mama na watoto leo tumefika hapa hospitali na kuwaona watu na sio kuwapatia afya lakini kushare upendo “sharifa
Ambrose Bikindo ni mdau kutoka QI Group of Company amesema kuwa siku ya wapendanao imekuwa nzuri kutokana na kuitumia kwa ajili ya watu wny mahitaji huku wakiahidi kuendelea kushiriki katika kuisaidia jamii .

“ Tumeweza kupata bahati kutembelea tosamaganga iringa mapokezi ni mazuri tumeweza kuwaona wamama waliojifungua kiukweli imekuwa ni furaha sana kujifungua na imekuwa faraja sana waliojifungua tareh 14 imekuwa ya kipekee sana na tutandelea kufanya social activities hata ukienda kwenye wbsite zao tumefarijika sana “

Ramadhan Ally ni moja ya vijan awalioshiriki katika siku hii ya wapeendanao amsma kuwa akiwa kama kijana amejifunza vitu vingi kutokana na hali waliyoikuta hospitali hapo huku akiikumbusha jamii kushiriki katika kuwasaidia wenye uhitaji kipindi hiki cha wapendanao .

“Nimefurahi sana maana ndo mara ya kwanza nawashukuru sana waliochangia kufika hapa unajua kwa nini nimefurahi nimewaza kwa hali tuliyoikuta huko ndani nimewaza hata mimi kuna siku ninaweza kuwa hapa ndani na by the way wagonjwa wamepata hope siku kama hizi kwangu zinapitaga tuu lakini siku kama ya leo watu hupeleka maua vitu wanavyopenda wapenzi wao lakini mimi nimeenjoy sana kuwa hapa leo ”

Siku ya wapendanao huadhimishwa kila tarehe 14/2 kila mwaka lengo likiwa ni kuikumbusha jamii kuhusu upendo huku watu wakiitumia siku hii kwa matukio tofautitofauti .
MWISHO