Nuru FM

Manispaa Ya Iringa Yaipongeza Kampuni Ya ASAS Kutwaa Tuzo Ya Ulipaji Kodi Bora

27 November 2022, 7:04 am

HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imeyaipongeza makampuni ya Asas kwa kupata tuzo ya ulipaji Kodi bora kutoka kwa mamlaka ya mapato(TRA) jambo linalosaidia kukuza uchumi wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada alisema kuwa Halmashauri makampuni ya Asas yamekuwa yanalipa Kodi vizuri na kuchangia maendeleo ya wananchi wa Halmashauri hiyo.

Ngwada alisema kuwa makampuni hayo yamekuwa yanalipa kodi kwa wakati bila kufanya ujanja ujanja wowote ule kwa mamlaka husika.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akizungumza na waandishi wa habari juu tuzo waliyopewa kampuni ya Asas kwa ulipaji bora wa Kodi kutoka TRA.

Alisema kuwa kulipa Kodi kwa makampuni hayo kunasaidia kulipa mishahara ya wafanyakazi wote wa serikali na kuchangia shughuli za kimaendeleo ambazo zitachangia kukuza uchumi wa Taifa.

Meya Ngwada alisema kuwa wafanyabiashara Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wamekuwa wanalipa bilioni moja na laki nane lakini Kati ya Kodi hiyo makampuni ya Asas yamekuwa yanalipa Kodi Kati ya Milioni mia nane hadi Milioni mia tisa.

“Katika kufanya kazi za kimaendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inategemea walipa Kodi kufanya shughuli za kimaendeleo na kukuza uchumi wa Halmashauri hiyo” alisema Ngwada.

Alisema kuwa wanaipongeza makampuni ya Asas kwa kuwa na mchango mkubwa wa kimaendeleo katika Manispaa ya Iringa Kwa kujenga majengo mbalimbali kama ofisi za meya wa Manispaa ya Iringa,jengo la ustawi wa jamii,ofisi za ardhi,jengo la watoto njiti,jengo la kuhifadhi damu salama,jengo la viongo bandia na misaada mingi kwa wananchi wa Manispaa ya Iringa.

Ngwada alimazia kwa kusema kuwa Wananchi na wafanyakazi wa Manispaa ya Iringa wanaendelea kuyapongoze Makampuni ya Asas kwa kupata tuzo ya ulipaji bora wa Kodi jambo ambalo linaleta sura nzuri kwa jamii.