Nuru FM

Mbunge Kabati aomba serikali kukarabati Barabara ya Mtandika kwenda ikula

11 April 2023, 11:32 am

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akiuliza Swali Bungeni. Picha na Hafidh Ally

Wanawake wajawazito wamekuwa wakipata shida wanapotaka kwenda kujifungua kutokana na ubovu wa Barabara hiyo.

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt. Ritta Kabati amehoji mpango wa serikali kukarabati Barabara ya Mtandika – ikula ambayo imekuwa kero kwa wananchi.

Dkt Kabati ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi Cha Maswali na Majibu na kuongeza kuwa wananchi haswa wajawazito wamekuwa wakipata changamoto wakati wa kwenda kujifungua huku akiiomba serikali kutenga fedha za kukarabati Barabara hiyo.

“Kwa kweli serikali ituambie ni lini wananchi wa wanaotumia Barabara ya Mtandika kwenda ikula wataanza kutumia Barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwao?”Alisema Kabati

“Kwa kweli serikali ituambie ni lini wananchi wa wanaotumia Barabara ya Mtandika kwenda ikula wataanza kutumia Barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwao?”Alisema Kabati

Amesema kuwa Barabara hiyo ya Mtandika kwenda ikula ni mbovu hasa kipindi Cha Mvua ambapo imekuwa hatarishi kwa uhai wananchi wa maeneo hayo.

Akijibu Swali hilo, Naibu Waziri wa nchi Ofisi Ya Rais TAMISEM Mh. Festo Dugange amesema kuwa serikali itafanya tathmini katika Barabara hiyo ili iweze kutengenezwa na kuwafikisha wananchi kupata huduma za afya.

Mh. Dugange Amesema baada ya tathmini hiyo serikali itatenga fedha za kukarabati Barabara hiyo ili wananchi waweze kuzifikia huduma za kijamii kwa wakati.