Nuru FM

Chamgogo Fc mabingwa wa Kiswaga Cup 2023

15 October 2023, 7:59 am

Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh Jackson Kiswaga akipeana Mkono na Mchezaji Bora wa mashindano Christopher Kidava. Picha na Hafidh Ally

Bingwa wa mashindano ya Kiswaga Cup ataelekea Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kufanya utalii kwa siku tatu.

Na Hafidh Ally

Timu ya Chamgogo Fc imeibuka Mabingwa wa Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Kiswaga Cup 2023 yanayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh Jackson Kiswaga.

Chamgogo Fc wamekuwa Mabingwa baada ya kuwafunga Kidamali Fc Goli 2-1 katika mchezo wa Fainali uliofanyika Katika Kijiji Cha Kalenga uliodhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jimbo la Kalenga.

Baada ya kuwa Mabingwa wa Mashindano hayo, timu hiyo ilikabishiwa zawadi ya Kombe na shilingi Milioni 1, Huku mshindi wa Pili Timu ya Kidamali Fc ikikabidhiwa shilingi Laki 8 na mshindi wa Tatu alikuwa ni Ugwachanya Fc ambao walikabidhiwa shilingi Laki 6 baada ya kuwafunga Muwimbi Fc Goli 4-0 katika mechi ya kutafuta Mshindi wa tatu.

Hata hivyo Mh. Kiswaga alitoa zawadi ya shilingi elfu 50 ya Kocha Bora ambayo ilienda kwa Kocha wa Chamgogo Fc Bw. Modelanus Kangalawe, Mchezaji Bora wa mashindano akiwa ni Christopher Kidava, huku zawadi ya Kipa Bora ikienda kwa Kipa wa Kidamali Fc Issa John na zawadi ya Timu yenye Nidhamu ikienda kwa Timu za Kikosi Kazi fc na Tagamenda Fc.

Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Veronica Kessy amezipongeza timu Zote zilizofika Fainali huku akiwataka Mabingwa kuendelea kuwa na Timu imara kwa ajili ya mashindano yajayo.

Awali Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh. Jackson Kiswaga amesema kuwa kwa sasa wanasubiria Utaratibu Wa kiwapeleka Mabingwa wa Mashindano hayo Zanzibar kutekekeza Ahadi ya Katibu wa Oganizesheni ya CCM Taifa Mh. Issa Gavu aliyotoa wakati wa Ufunguzi wa mashindano na Kisha kumalizia kwa safari ya Dodoma.

Mashindano hayo yalienda sambamba na michezo ya jadi kama Draft na Bao(solo) kwa ajili ya Kumbukizi ya Miaka 24 ya kifo Cha Baba wa Taifa Mwalimu Julia’s Kambarage Nyerere ambapo washindi wa Michezo hiyo walikabidhiwa shilingi elfu 50 kila Mmoja.