Nuru FM

Mgomo wa daladala Iringa waingia siku ya pili

7 May 2024, 8:35 pm

Picha ya Mwonekano wa Stand ya daladala Manispaa ya iringa baada ya daladala kugoma. Picha na Hafidh Ally

Mgomo wa madereva daladala umechukua sura mpya baada ya madereva hao kutotoa huduma ya usafiri kutokana na Madereva bajaji kuingilia Njia zao.

Na Hafidh Ally

Madereva daladala katika kituo cha stand ya zamani ya mabasi Manispaa ya Iringa wameendeleza mgomo wa kutoa huduma ya usafiri kwa siku ya pili.

Wakizungumzia sababu ya kufanya Mgomo huo, baadhi ya madereva daladala wamesema kuwa kumekuwa na tabia ya madereva bajaji kuingia katika kituo chao na kuchukua abiria kinyume na makubaliano waliyowekeana.

Sauti ya madereva Daladala

Kwa upande wao baadhi ya abiria manispaa ya iringa wamesema kuwa mgomo wa daladala unawafanya watumie gharama kubwa wanaposafiri.

Sauti ya Abiria

Nao baadhi ya madereva Bajaji manispaa ya iringa wamesema kuwa mgomo wa daladala imekuwa fursa kwao na wanaweza kutoa huduma ya usafiri bila changamoto.

Sauti ya Madereva Bajaji

MWISHO