Nuru FM

Timu ya Simba SC yaomba radhi hadharani

11 August 2022, 7:31 am

Klabu ya Simba inaomba radhi kwa waumini wa dini ya Kikristo, viongozi wa madhehebu yote ya Kikristo, Serikali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania na jamii kwa ujumla kwa usumbufu uliojitokeza kwenye tamasha letu la Simba Day Agosti 8 mwaka huu.

Katika tamasha hilo msaniii Khalid Ramadhani Tunda maarufu “Tundaman” aliingia uwanjani kutumbuiza ambapo alitumia mavazi, vifaa na ishara ambavyo vimeibua hisia na kuwakera wengi hasa waumini na viongozi wa dini ya Kikristo.

Kwa kuheshimu imani za watu wote tumelazimika kuomba radhi kwa tukio hilo.

Hata hivyo kabla ya onyesho hilo, Simba hatukufahamu kama Tundaman atatumia aina hiyo ya maudhui kwani siku ya majaribio hakufanya hivyo.
Vile vile tumewataka wasanii hao waombee radhi kwa jamii ambapo wamekiri na kuahidi kufuata taratibu stahiki katika kuomba radhi na kujutia kosa hilo.