Nuru FM

Wizi wa mifugo washamiri Kiwele

2 May 2024, 10:00 am

Picha ya Mifugo mbalimbali inayofugwa na wananchi kwa lengo la kujiinua kiuchumi. Picha na Hafidh Ally

Wananchi wa Kata wa Kiwele wametaka kukomeshwa mara moja tabia wizi wa mifugo unaofanywa na vijana wenye nia mbaya.

Na Joyce Buganda

Wimbi la wizi wa mifugo limeshika kasi katika Kijiji na kata ya kiwele Halmashauri ya Wilaya ya Iringa jambo ambalo ni tishio kubwa katika kata hiyo.

Wakizungumza kijijini hapo wafugaji hao wamesema wanaibiwa mifugo yao kutoka vijiji vya jirani hivyo kuiomba serikali iwasaidie kukomesha tabia hiyo.

Aidha Diwani wa kata ya Kiwele FELIX WAYA amesema ni vyema wafugaji hao wakaanzisha umoja wao ili kuepukana na changamoto hiyo.

Hata hivyo diwani Waya amewasisitiza wafugaji hao kuwa na ushirikiano baina yao ikiwa ni pamoja na kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzie.

MWISHO