Nuru FM

Bukumbi acharuka kampuni za Ulinzi zisizolipa wafanyakazi

21 May 2026, 08:44

SACP Allan Bukumbi akizungumza na Viongozi wa Kampuni Binafsi za Ulinzi Mkoani Iringa. Picha na Ayoub Sanga

Jeshi la Polisi limebaini kuwa kampuni nyingi zinaendesha shughuli zake kinyume cha sheria.

Na Ayoub Sanga

Jeshi la Polisi mkoani Iringa limetangaza kiama kwa kampuni za ulinzi ambazo zimekuwa zikikiuka sheria na kanuni za vibali vya ulinzi, hali inayodaiwa kusababisha malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa wananchi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Allan Bukumbi amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya wamiliki wa kampuni za ulinzi kuajiri watu wasio na vigezo sambamba na kuwapa silaha bila kuwapatia mafunzo stahiki sambamba na kuwacheleweshea mishahara wafanyakazi wao.

Sauti ya Kamanda

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Kampuni Binafsi za Ulinzi Tanzania (TISIA) Mkoa wa Iringa, Alexander Mkumbo amekiri kuwa ukosefu wa mshikamano na ushirikiano miongoni mwa kampuni binafsi za ulinzi umekuwa chanzo cha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo mkoani Iringa.

Sauti ya Mkumbo

Nao Polisi Kata Jamii Wilaya ya Iringa wamesema kuwa licha ya kufanya kazi kwa karibu na Kampuni Binafsi za ulinzi bado kumekuwa na changamoto za kutoheshimiwa na watendaji wa Kampuni hizo.

Sauti ya Polisi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limeeleza kuwa hatua hizo zinalenga kuhakikisha sekta ya ulinzi binafsi inafanya kazi kwa kuzingatia sheria, taaluma na usalama wa wananchi .