Nuru FM
Nuru FM
2 May 2026, 20:32

Wahitimu wa Kidato Cha Sita katika shule ya Sekondari JJ Mungai iliyopo Halmashauri ya Mji Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa kuisaidia Jamii Kwa kutumia Elimu yao.
Ma Fredrick Siwale
Hayo yamezungumzwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa (UoI) Dr.Salvatory Mhando katika Mahafali ya 20 kwa Wahitimu wa Shule ya Sekondari J. J. Mungai iliyopo Halmashauri ya mji Mafinga na kuongeza Kuwa Wahitimu hao wanapaswa kutumia Elimu yao katika kufanya Shughuli za kiuchumi na kijamii ili kukuza uchumi na kujiingizia kipato.

Aidha Amewataka wazazi kuwaombea Dua watoto wao kufanya vizuri katika mitihani ambayo wanatarajia kuifanya mapema mwezi huu.
Akisoma taarifa ya Shule hiyo Mwl. Nashon Boniface Ndanzi amesema mwaka 2026 wana Jumla ya Wahitimu 137 na kati yao Wavulana ni 70 na Wasichana ni 67.
Mwl. Ndanzi amesema kwa ujumla maendeleo ya elimu na Wanafunzi katika shule hiyo ni mazuri na Uongozi unaamini kuwa watafanya vizuri zaidi katika mitihani yao.
Akizungumza kwa niaba ya Wazazi Bw. Vicent Chota aliwashukuru Waalimu kwa malezi mazuri na kusimamia nidhamu iliyopelekea shule hiyo Kuwa na matokeo mazuri.