Care Tanzania yaleta usawa katika Jamii Iringa
19 May 2026, 09:17

CARE Tanzania imesaidia kwa kiwango kikubwa kutoa elimu kwa wakazi wa vijiji vya Holo, Kibebe na Ulanda.
Na Adelphina Kutika
Shirika la CARE Tanzania limetoa mafunzo ya kusaidiana majukumu ya nyumbani kwa wananchi wa kata za Ulanda na Kibebe katika Wilaya ya Iringa, ili kumpatia mwanamke nafasi ya kupumzika na kuimarisha maendeleo ya kaya.
Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyodumu kwa takribani siku tatu vijijini humo, Mkurugenzi na Meneja Mwandamizi wa Uchangiaji Fedha wa CARE Tanzania, Christina John, amesema lengo la mafunzo hayo ni kubadilisha mitazamo hasi ya mila na desturi zinazompa mwanamke jukumu lote la kazi za nyumbani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Steven Mhapa, amelipongeza shirika la CARE Tanzania kwa juhudi zake za kuwajengea wananchi uwezo katika nyanja mbalimbali.
Naye Mwinyikheri Kharifa Polisi Kata ya Ulanda amewahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pindi matukio ya uhalifu au vitendo vya ukatili .
Nao Baadhi ya wananchi waliopatiwa mafunzo hayo wamesema elimu ya jinsia imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii, hasa katika kubadili mtazamo wa baadhi ya wanaume waliokuwa wakiamini kuwa jukumu la kulea watoto na kufanya kazi za nyumbani ni la wanawake pekee.SAUTI 4 WANANCHI
