Nuru FM
Nuru FM
12 December 2025, 12:05

“Fedha hizi zitumike kwenye kuleta maendeleo ambayo mmeyaandikia kwenye miradi yenu”
Na Hafidh Ally
Jumla ya vikundi 71 vinavyoundwa na wananchi wanaojishughulisha na kilimo, ufugaji na viwanda vidogo katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa wamepata mikopo ya Asilimia 10 yenye thamani ya Shilingi Milioni 407.9.
Mkuu wa Idaya ya Maendeleo Wilaya ya Iringa Saumu Mweka amesema kuwa Mikopo hiyo imetolewa kama sehemu ya mkakati wa Serikali kuwajengea uwezo wa kiuchimi wananchi na kuongeza ushiriki wao kwenye shughuli za uzalishaji mali hususani vijana, wanawake na wenye ulemavu na ikitarajiwa kuchochea ongezeko la uzalishaji, kukuza ajira na kuinua vipato vya wanufaika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Benjamini Sitta amesema kuwa fedha zilizokabidhiwa kwa vikundi hivyo zinapaswa kupelekwa kwa kwenye miradi iliyokusudiwa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amewataka wananchi kutokopa fedha za Halmashauri kama huna shughuli za Kufanya ambapo mkopo huo siyo wa riba.
Mikopo hiyo inatarajiwa kuchochea ongezeko la uzalishaji, kukuza ajira na kuinua vipato vya wanufaika katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo hasa yale yaliyopo pembezoni.