Mwigulu: “Wananchi Iringa wasiuziane ardhi kiholela”
8 June 2026, 09:57

Viongozi mliopo hapa waambieni wananchi hivi sasa masuala ya ardhi wasifanye kwa kuaminiana, wawe wanaandikishana kwa mikataba na tena katika ofisi za kijiji ili watambulike.
Na Hafidh Ally
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba amewataka watumishi na Viongozi Mkoani Iringa kutoa elimu ya masuala ya ardhi ili kupunguza migogoro.
Mh. Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza na viongozi wa kada mbalimbali wa mkoa wa Iringa katika kikao cha majumuisho ya ziara zake kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, mjini Iringa na kuongeza kuwa ni vyema wananchi wasiuziane ardhi kwa kuaminiana na badala yake waandikishishiane katika ofisi za kijiji kwa mikataba ya mauziano.

Mh. Mwigulu Nchemba amesema kuwa wananchi wasiogope kurasimisha ardhi zao kwani uaminifu umepungua katika jamii jambo ambalo litasaidia wakati changamoto za ardhi zinapojitokeza.
Amesema Serikali itaendelea kufanya tathmini ya utekelezaji wa maelekezo hayo na kwamba viongozi wa mikoa na halmashauri wanapaswa kuweka kumbukumbu za utekelezaji wa kila hoja iliyowasilishwa na wananchi.