Nuru FM

Kundo: Wakandarasi wazawa wapewe kipaumbele

12 December 2025, 12:06

Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Mhandisi Andrea Kundo, akiwa Halmashauri ya Mji Mafinga katika ziara. Picha na Hafidh Ally

Utekelezaji wa majukumu yenu unapaswa kuzingatia mkataba ili kutatua kero ya maji kwa wananchi”

Na Hafidh Ally

Wandarasi wazawa (wa ndani ya Nchi), wametakiwa kutanguliza uzalendo wanapotekeleza Ujenzi wa miradi ya Maji wanayopewa na Serikali  ili kutatua kero ya maji katika jamii.

‎Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Mhandisi Andrea Kundo, akiwa Halmashauri ya Mji Mafinga Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa katika Ziara yake ya Ukaguzi wa hali ya utekelezaji wa mradi wa Maji wa miji 28, ambapo Mafinga ni Moja ya Mji ambao umefikiwa na mradi huo wa kitaifa unaolenga kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji safi Kwa Wananchi.

Sauti ya Kundo

Aidha Mhandisi Kundo amesema kuwa kama serikali inatoa fedha na kazi haifanyiki kwa ufasihi italazimu kupitia mkataba walioingia na Mkandarasi ili kukukumbushana utekelezaji wake.

Sauti ya Kundo

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mkoani Iringa, Dickson Lutevele (Villa), amewasilisha kero ya uhaba wa Maji Safi inayowakabili Wananchi wa Jimbo hilo, huku akiomba Mji wa Mafinga upewe Kipaumbele na nguvu zaidi iongezwe ili kutatua kero hiyo hasa Kupitia Mradi wa Kitaifa wa Maji wa Miji 28 unaolenga kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji safi Kwa Wananchi waishio mijini.

Sauti ya Mbunge

Mradi wa Mafinga ni sehemu ya mpango wa kitaifa unaolenga kuongeza huduma ya maji mjini Mafinga na Utekelezaji wake unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 48.