Nuru FM

Bilioni 64 kujenga barabara ya ipogolo-Kilolo

11 May 2026, 13:19

Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Nzelemela akizungumza kwenye Baraza la Madiwani. Picha na Hafidh Ally

Barabara zinazotengenezwa Wilaya ya Kilolo zinatarajia kukuza uchumi wa wananchi wa eneo hilo.

Na Hafidh Ally

Zaidi ya Bilioni 64 zimetumika kufanya Ujenzi wa barabara ya Ipogolo hadi Wilaya ya Kilolo inayotarajiwa kuwa chachu muhimu ya maendeleo kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza baada ya kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika ofisini kwake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Rashid Ramadhani Nzelemela, amesema barabara hiyo itarahisisha kwa kiasi kikubwa shughuli za usafirishaji.

Sauti ya Nzelemela

Aidha amesema kuwa serikali itafunga taa kuanzia Ipogolo Hadi Wilaya ya Kilolo jambo litakalowasaidia wakulima kusafirisha mazao yao na masoko kwa urahisi zaidi.

Sauti ya Nzelemela

Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema kuwa wameshawasiliana na Tanroad kwa ajili ya kuwaomba kurekebisha baadhi yabarabara za vumbi zilizopo katika Wilaya hiyo ili kurahisisha usafiri na mawasiliano kati ya wananchi wa maeneo mbalimbali.

Sauti ya Nzelemela

Kwa upande wao, baadhi ya madiwani wa Halmashauri hiyo wamepongeza juhudi za serikali katika utekelezaji wa mradi huo, wakieleza kuwa barabara hiyo itakuwa na mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo ya Wilaya ya Kilolo.