Nuru FM

Mtatifikolo: Nipo tayari kuwatumikia Wanaismani

13 May 2026, 11:40

Mgombea wa Ubunge Jimbo la Isman Emmanuela Mtatifikolo akinadi sera zake. Picha na Hafidh Ally

Na Hafidh Ally

Wananchi wa Tarafa ya Pawaga Kata ya Itunundu Wilaya ya Iringa Vijijini wamejitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Isimani kupitia Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Emmanuela Mtatifikolo.

Wananchi hao wameeleza kuwa na imani kwa Mgombea Ubunge huyo Bi. Emmanuela Mtatifikolo katika kuleta Maendeleo na kukuza uchumi wa Wananchi wa Jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kampeni hizo Bi. Mtatifikolo amesema kuwa atahakikisha wananchi wa jimbo hilo wanapata maendeleo kwa kuendeleza agenda zilizoanzishwa na mtangulizi wake Hayati Wiliam Lukuvi zikiwemo sikimu ya umwagiliaji, na ujenzi wa barabara ya Iringa mpaka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Sauti ya Mtatifikolo

Naye Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh. Jackson Kiswaga ambaye alishiriki kumnadi mgombea huyo amewataka wananchi kumpigia kura jwa wingi Bi Mtatifikolo kwani ni kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza na kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Katika hatua nyingine, viongozi waliokuwa wamejitokeza kuwania ubunge kupitia kura za maoni za CCM walionesha mshikamano kwa kuungana kumuunga mkono mgombea huyo.

Iringa inafanya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Ismani baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, marehemu William Lukuvi ambapo Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Juni 1, 2026.