Nuru FM

Mradi wenye thamani ya Dola Mil 15 wa kiwanda Cha Mazao ya misitu Mafinga wawekewa jiwe la Msingi

6 May 2023, 2:23 pm

Viongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa. Picha na Ansgary Kimendo

Na Ansgary Kimendo

Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa kiwanda cha kuchakata masalia ya misitu iliyovunwa umezundua cha Lush chazo wood industries Ltd wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 15

Katika uwekaji jiwe lamsingi huo kipngozi wa mbio za mwenge kitaifa RAMADHAN SHAIB KAIM amewapongeza wawekezaji wakiwanda hicho pamoja na kuwataka Halmashauri ya mji wa mafinga kuhakikisha waajiliwa wa kiwanda hicho wanapata maslahi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuangalia mikataba.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mafinga mhe. Kosato chumi ameziomba mamlaka husika kuhakikisha bidhaa zinazo zalishwa kiwandani hapo zinaandikwa kuwa zinazalishwa mkoani iringa nchini Tanzania.

Nae Hassan makoba katibu Uvccm mji wa Mafinga amesema uwepo wa kiwanda hicho unachochea fursa za ajira kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo mengine.

Viongozi wakiwa wanatembelea cha Lush chazo wood industries Ltd.

Katika hatua nyingine mwenge wa Uhuru umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika mji wa Mafinga ikiwemo Kituo cha mafuta NFS, Mradi wa jengo la huduma za dharura katika hospital ya mji Mafinga ujenzi wa barabara, uzinduzi wa jengo la maabara katika shule ya upendo pamoja na upandaji wa miti.