Nuru FM

RC mpya Iringa ahimiza weledi

12 March 2024, 11:22 am

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akikabidhiwa ofisi na Mh. Halima Dendego ambaye amehamishiwa Mkoa wa Singida. Picha na Ayoub Emanuel.

Watumishi wazembe katika ofisi za umma waonywa ili kuleta maendeleo mkoani Iringa.

Na Godfrey Mengele

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amewataka watumishi waliopo katika idara mbalimbali kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma kwa jamii na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Peter Serukamba ameyasema hayo wakati wa Makabidhiano ya Ofisi na Mkuu wa Mkoa aliyepita Halima Omary Dendego na kuongeza kuwa katika uongozi wake hapendelei kuona watumishi wanapeleka majungu kwake kwani hata vumilia na hayupo tayari kutunza siri ya aliyepelekewa majungu.

Mkuu mpya wa Mkoa wa Iringa Peter Joseph Serukamba, amepokelewa na kukabidhiwa rasmi ofisi, vitendea kazi pamoja na kutambulishwa kwa viongozi wengine wa Serikali ya mkoa huo, viongozi wa ulinzi na usalama, viongozi wa Dini pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoani humo ambapo kabla ya uhamisho Peter Serukamba alikiwa mkuu wa Mkoa wa Singida.