Nuru FM

Lyra in Afrika wakabidhi bweni na kompyuta shule ya Mseke

23 February 2024, 9:50 am

Bweni lililojengwa na Lyra in Afrika katika shule ya sekondari Mseke. Picha na Godfrey Mengele.

Na Godfrey Mengele

Shilingi million 246 zimetumika katika ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mseke iliyopo kata ya Masaka halmashauri ya wilaya ya Iringa ili kupunguza adha ya wanafunzi wa kike kutembea umbali mrefu.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya bweni hilo pamoja na kompyuta 32 katika shule hiyo Meneja Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa CK Richards amesema shirika ,wananchi na wadau wengine kuwa kwa kutambua changamoto hiyo wameamua kujenga bweni ambalo litawasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao.

Sauti ya Mkurugenzi wa Lyra in Africa CK Richards

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Bi Veronica Kesy akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa amelishukuru Shirika la Lyra In Afica kwa kufanikisha ujenzi  wa bweni hilo  kwani baadhi ya wanafunzi wa kike wamekuwa hawafikii malengo yao na changamoto kubwa ni umbali wanaofuata elimu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Bi Kessy

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari mseke amelishukuru shirika la Lyra in Africa kwa ujenzi wa bweni hilo pamoja na msaada wa computer ambao utawasaidia wanafunzi wa kike kusalia shuleni na sasa ufaulu utaongezeka huku akibainisha na changamoto nyingine zinazohitajika kutatuliwa.

Sauti ya Mkuu wa shule