Nuru FM

Mbunge Kabati aibana serikali, ataka irekebishe Mfereji wa maji Ruaha Mbuyuni.

28 April 2023, 3:36 pm

Mbunge Kabati akiuliza Swali Bungeni Jijini Dodoma. Picha na Halfan Akida.

Na Halfan Akida

Mbunge viti maalum mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati ameitaka serikali kuchukua hatua za dharura kuwasaidia wananchi wa Ruaha Mbuyuni baada ya mfereji wa maji kuacha njia yake na kuathiri wakulima

Kabati amehoji hayo katika kipindi cha maswali na majibu kwa wizara ya Kilimo leo bungeni Jijini, Dodoma.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Kilimo, Mh Hussein Bashe amesema serikali inatambua tatizo hilo la mfereji kuacha njia yake katika eneo la Ruaha Mbuyuni, wilaya ya Kilolo.

Amesema serikali imetuma wataalamu kutoka wizara ya Kilimo kwenda katika eneo hilo kuona namna ya kuondoa changamoto hiyo.

Waziri Bashe ameongeza kuwa tatizo hilo lilipo Kilolo linafanana na tatizo lililokuwepo Mlenge na Mkombozi ambako kila Mwaka mvua zikiwa nyingi mto huacha njia.

Amesema serikali imeamua kufanya usanifu upya eneo hilo ili kuondoa kabisa tatizo hilo.