Nuru FM

Wananchi wamtaka mwenyekiti kujiuzulu kwa matumizi mabaya ya ofisi

18 May 2021, 8:26 am

Wananchi wa Kijiji cha Ikuvilo Kata ya Luhota Wilaya ya Iringa wamemtaka mwenyekiti wa Kijiji chao Herman Mkini kujiuzulu nafasi yake kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya Ofisi.

Wakizungumza katika mkutano wa Hadhara mmoja wa wananchi wa kijiji hicho Petro Kisinda amesema kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa Mwenyekiti huyo kutokana na kutumia vibaya fedha za wanakijiji.

Wananchi hao wamesema kuwa Mwenyekiti amekuwa akitumia vibaya fedha za mapato ya kijiji ambazo zinapitia mikononi na mwake na amekuwa hatoi taarifa za matumizi yake.

Wamesema kuwa ili kijiji kiweze kupiga hatua kimaendeleo ni vyema mwenyekiti huyo akaachia madaraka ili waweze kupata kiongozi mwingine ambaye atawasaidia katika kuleta maendeleo.

Akijibia tuhuma hizo Mwenyekiti wa Kijiji hicho HERMAN MKINI amesema kuwa fedha zilielekezwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo ukarabati wa jengo la ofisi.

Kwa upande wake Diwani ya Luhota Bw. Bruno Kindole amesema kuwa wananchi wa kijiji hicho wanatakiwa utaratibu wa kumuondoa mwenyekiti madarakani.