Nuru FM

Wahitimu msitegemee ajira – Prof. Anangisye

21 December 2020, 9:05 am

Wahitimu wa Fani mbalimbali katika Chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa kilichopo mkoani Iringa wametakiwa kutumia Taaluma zao katika kuongeza thamani ,Ubunibu  na Kutengeneza Ajira zitakazoinufaisha jamii inayowazunguka badala ya Kutegemea kuajiriwa.

Akizungumza na Katika Mahafari ya 12 ya Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu Mkwawa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Chuo hicho na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salamu Prof. Willium Anangisye na PROF. ESTER DUNGUMALO ambaye ni RASI WA CHUO MKWAWA wamesema kutokana na Ufinyu wa Ajira kwa sasa ni vyema wahitimu kuwa wabunifu ili kujitengenezea Ajira.

Sauti ya Prof. Anangisye na PROF. Dungumalo

Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salam Mwanaidi Mtanda ameeleza baadhi ya Changamoto zinazokwamisha baadhi ya Malengo ya Utoaji elimu kwa Ufasaha katika Chuo hicho kuwa ni pamoja uhaba wa wahadhiri wa fani mbalimbali.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa baraza la chuo cha UDSM

Akisoma Risala ya wahitimu wa chuo hicho, Mhitimu wa Shahada ya Elimu katika Elimu ya Jamii JULIAS THOMAS amesema kuwa bado kuna uhaba wa maktaba na malazi.

Sauti ya Julius Thomas

Katika mahafali hayo Jumla ya wanafunzi 1938 wamehitimu katika chuo hicho huku wito ukitolewa kwao kuhakikisha wanakuwa chachu ya Maendeleo katika Maeneo yao.

Picha na Wikimedia Commons