Nuru FM

Kabati awasilisha bungeni changamoto ukosefu maji Ng’ang’ange

8 June 2023, 11:09 am

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akiuliza swali bungeni jijini Dodoma. Picha na Hafidh Ally

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ameibana serikali kujua wana mpango gani wa kupeleka huduma ya maji katika kata ya Ng’ang’ange iliyopo wilaya ya Kilolo.

Kabati ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu na kuongeza kuwa wananchi wa kata hiyo wamekuwa wakitumia maji ya mito ambayo siyo salama kwao huku akitaka kujua serikali itatenga lini fedha za mradi wa maji.

Akijibu swali hilo bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mh. MarryPrisca Mahundi amesema kuwa wizara yake inatambua changamoto hiyo na watapeleka mashine kwa ajili ya kuchimba visima.

Aidha amesema kuwa kisima kitachimbwa katika mwaka ujao wa fedha 2023/2024.

Mh. MarryPrisca amempongeza Mh. Kabati kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto za wananchi wa mkoa wa Iringa.